Mahitaji
Karanga kilo 1
Yai moja
Mafuta ya kula ( ya maji ) mls 750
Sukari vijiko 6 vya chakula
Unga wa ngano kikombe kimoja cha kahawa( coffee cup)
Chumvi ya unga nusu kijiko cha chai.
Jiko
Chombo –Sufuria/bakuli
Mwiko /kijiko kikubwa
Maelekezo
Chukua yai, pasua na koroga kwenye chombo kisafi.
Chukua karanga,mimina kwenye chombo ulicho koroga yai ,changanya kwa kutumia mikono.
Weka chumvikidogo, changanya vizuri, weka sukari changanya, mimina unga wa ngano, changanyavizuri.
Weka mafuta jikoni hadi yapate moto.
Chota karanga kwa kutumia kijiko kikubwa na weka kwenye mafuta kisha zigeuze bila kuacha hadi utakapoona karanga zimebadilika rangi kua kahawia.
Tumia kijiko kikubwa kuziepua na weka kwenye chombo kisafi cha wazi ilizipoe.
Funga kwenye vifuko vidogo na zihifadhi mahali pasafi tayari kwa kula au kuuza.
No comments:
Post a Comment