Sambusa za nyama
- Nyama steki kilo 1
- Vitunguu maji 2
- Majani ya Giligiliani vifungu 2
- Garam masala kijiko 1 cha chai
- Chumvi kijiko 1 cha chai
- Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
- Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
- Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
- Karoti 2 kubwa
- Pilipili hoho 2
- Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
- Manda
- Butter
Maelekezo
- Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
- Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
- Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
- Chukua frying pan pana, weka butter. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
- Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
- Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala koroga dakika 2, epua. Usiifunike
- Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
- Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
- Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
- Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia kisha unaepua zinakuwa tayari kwa kuliwa
No comments:
Post a Comment