Total Pageviews

Tuesday, April 16, 2019

Biashara rahisi kuzifanya na kukuletea mafanikio mazuriii,By Diana Morsad




Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyafanya bila mtaji kabisa na mengine ambayo unaweza kufanya kwa kutumia mtaji mdogo sana ambao nirahisi kupatikana. Hapa nimejaribu kuchambua baadhi tu ya mambo ili kukupa mwanga, nimeangalia mambo ambayo kiuhalisia yanawezekana katika mazingira yatu.
Kitu cha muhimu hapa kabla ya kuanza biashara yoyote ni kuangalia mazingira yako, angalia kama wazo lolote la biashara ambalo unalo kichwani linawezekana katika mazingira yako. Kama haliwezekani basi usikomae nalo sana, angalia linalowezekana katika mazingira yako na anza na lo hilo.
Nilichoandika hapa ni mifano michache kutokana na tafiti nilizofanya mimi, fanya tafiti zako na chukua mifano hii iweke katika mazingira yako kisha ifanyie kazi. Mifano ni mingi sana, fursa ni nyingi sana ambazo siwezi kuziandika zote, tumia mifano hii kama kitu cha kukuzindua kuangalia fursa zinazokuzunguka, jiongeze.
(1) BIASHARA YA KUUZA NGUO
Biashara ya nguo ni moja ya biashara ambazo binafsi naamini ni rahisi sana kuanzisha, hii inatokana na ukweli kuwa kila mtu anahitaji kuvaa na kustirika na kila siku mitindo mipya ya nguo hujitokeza. Unaweza kuanzisha biashara hii kwa kutumia njia karibu zote nilizozitaja hapo juu.
Unaweza kuanzisha kwa kutumia sample, hapa unaweza kununua nguo chache na kuzipitisha kwa majirani zako kuwaonyesha, kupitisha maofisini na kuweka kwenye mitando ya kijamii. Watu watakapoweka oda basi ukaenda kuwanunulia na hapo utakuwa mwanzo wa biashara yako.
Lakini pia unaweza kuwa dalali wa nguo, wa kutafuta wateja kwaajili ya duka flani kwa kuweka nguo zao katika mitando ya kijamii, kutengeneza vipeperushi na kila mtu anaponunua kupitia wewe ukapata kamisheni. Nguo pia unaweza kuziuza kupitia mitando ya kijamii tu, kwa kutengeneza duka lako huko na wewe kuwa kama muuzaji.
Kama nilivyokwisha sema huko awali watu wanaweka oda na kulipia kabla. Hivyo unaweza kuanzisha ukurasa maalum katika mitando yako ya kijamii, ukaipa jina biashara yako na hata kuanzisha blog ambayo utakuwa ukitundika nguo mbalimbali, bei zake na mawasiliano yako.
Hapa watu wakawasiliana na wewe, wakaoda nguo na wewe kuwapelekea majumbani mwao, vyuoni, maofisini au kuwatumia kwa njia za mabasi. Unaweza kuuza nguo, viatu, mikoba, mabegi, mikanda, pochi manukato, mashuka na vitu vingine vingi kwa njia hii na kufanikiwa.
Unaweza kuanza hivi ukiwa na malengo ya kukua mpaka kumiliki duka lako mwenyewe la nguo, au kubakia kuwa muuzaji wa nguo katika mitandao, yote haya yanawezekana ingawa ni muhimu mwisho wa siku kuwa na malengo ya kumiliki ofisi, sehemu ambayo wateja wako wanaweza kukupata wakiwa na matatizo.
Biashara ya nguo ambayo umeianzisha kwa kuzungusha nguo chache za mifano katika maofisi, umeianzisha kwa kuweka picha tu katika mitandao ya kijamii unaweza kuw ana malengo ya kumiliki duka kubwa la nguo, mini shopping mall au shoping mall kabisa, kitu cha muhimu nikuwa na malengo mazuri.
(2) BIASHARA YA KUUZA SIMU ZA MIKONONI
Hii ni biashara nyingine ambayo unaweza kuianzisha hapo ulipo. Unaweza kuanza kwa kuuza sample za simu, kwa mfano kama una simu nzuri unaweza kuanzia hapo. Jitambulishe kwa marafiki zako na watu wako wa karibu kama muuza simu hata kama hujawahi kuuza simu.
Mtaji wa simu unaweza kua mkubwa kidogo, hasa kama utataka kutumia njia ya sample, kwa maana watu watataka waone. Hapa ndipo unaweza kuanza kwa kusambaza sample za vitu vidogo au kuuza vitu vidogo vidogo, kama vile chaja za simu, power bank na makasha ya simu.
Ukianza kuzungusha vitu hivi moja kwa moja watu watahisi unajishughulisha na simu na hapo ndipo utawaambia biashara yako. Download picha za matoleo mapya ya simu, au nenda kabisa kwa wauzaji wa simu wa jumla na piga picha simu au chukua vipeperushi kisha anza kujitangaza.
Tumia mitandao ya kijamii kuweka picha za simu na bei zake, anza kuuza kwa marafiki zako. Unaweza pia kuanza biashara hii kwa kuwa kama wakala wa brand flani ya simu, wafuate na kuwaomba vipeperushi na picha kisha anza kutafuta wateja, anza kwa marafiki zako, ndugu zako, wafanyakazi wenzako na katika mitando ya kijamii.
Ukiweza kuwashawishi wateja na kuuza simu mbili tatu wanaweza kukuamini kama wakala wakakutumia kujitangaza na kuuza simu zao kupitia wewe. Nguvu yako ya ushawishi ndiyo itaweza kukusaidia hapa kuweza kupata wateja wengi na kutengeneza pesa zaidi lakini pia kuweza kuaminika na wauzaji halisi wa simu.
Unaweza kufungua kakibanda kadogo na kuweka vifaa vidogo vidogo vya simu ambavyo havihitaji kabisa mtaji mkubwa, unaweza kuanza kutangaza simu yako mwenyewe, kuwaonyesha marafiki zako na kujitangaza kama muuzaji wa simu.
(3) BIASHARA YA KUUZA CHAKULA
Anza kwa kupika vitafunwa na kuviuza kwa majirani wanaokuzunguka. Kama unajua kupika chapati nzuri, vitumbua, maandazi na vitu vingine kama hivyo basi anza kwa kupika na kuwauzia majirani. Hii ni fursa kubwa kwani ni watu wachache sana hupika vitafunwa asubuhi, wengi hununua.
Pika vitafunwa vyako vizuri na vifunge kwa usafi kisha anza kusambaza kwa majirani asubuhi. Vipaki vizuri ili kuwa tofauti na yule ambaye hupeleka katika duka la jirani, huku ukiongeza ubunifu wa uwapelekea watu asubuhi majumbani mwao. Kwa maana kuwa usisubiri watu kuja kuchukua pika na sambaza majumbani.
Unaweza kuvipaki katika makundi, kwa mfano kundi la vitafunwa vya shilingi mia tano, elfu moja na kuendelea. Hii inamlazimisha mnunuzi kununua vingi na kubwa zaidi vinakuwa katika vifungashio vizuri na visafi ambavyo vitamvutia mlaji.
Huu kwako ni mwanzo, peleka chakula maofisini, kuna ofisi ambazo hupikia watumishi wao chakula na nyingine hazifanyi hivyo, pika chakula cha sample weka fungasha vizuri kisha wapelekee ofisini kuonja kwaajili ya kuweka oda ya chakula chenyewe, kama ni kizuri na hawapikiwi nina uhakika utapata wateja wakuweka oda.
Usiishie tu kuwaza kuuza chakula cha mgahawa, jipanue kuwaza kupika kwenye sherehe. Kuna sherehe nyingi ambazo huandaliwa, jitangaze kama mpishi, peleka sample kwa kamati za sherehe kuwaonyesha chakula chako, tengeneza vipeperushi na wapelekee.
Anza kujitangaza katika mitando ya kijamii. Kwa maana kuwa tafuta jina la biashara yako na anza kulitumia katika mitando ya kijamii kutangaza huduma unazotoa. Unaweza kusema unapokea tenda za chakula maofisini, watu binafsi, sherehe na matukio mbalimbali. Pika chakula chako na piga picha kisha kuwa unaziweka katika mitandao ya kijamii.
Hapa nashauri usiweke picha feki bali picha za chakula unachopika wewe. Huhitaji kupika vyakula vingi na kuvipiga picha bali unaweza kupika chakula cha nyumbani kwako tu na kukipiga picha. Nikimaanisha kuwa kila unapopika chakula kipakue vizuri piga picha na zikusanye kwaajili ya matangazo.
Kwa mfano kama leo umepika wali kuku, upike vizuri, upakue vizuri na upige picha, ukipika ugali fanya hivyo hivyona vyakula vingine. Tengeneza profile ya vyakula na itumie kujitangaza, chapisha vipeperushi vya vyaula vyako na tangaza kwa watu, katika mitando na makundi ya Watsapp.
Kwa maana hiyo katika wazo hili unaweza kuwa na malengo ya kufungua mgahawa ambapo utaanza kwa kupikia watu wakaribu na maofisi ya karibu, lakini pia ukawa na malengo ya kufungua kampuni kwaajili ya kupika kwenye matukio ambayo utajitangaza kwenye sherehe na matukio mbalimbali kupitia mitando ya kijamii au ukafanya vyote kwa pamoja.
Lakini pia unaweza kufanya vyote kwa pamoja. Unaweza kutumia njia ya sample, ukawa dalali wa kampuni ya kupika vyakula katika sherehe kwa kuwatafutia shughuli za kupika, ukawa unapika bites na kuzisambaza katika mashule na mtaani, lakini pia ukapika chakula na kuuza kando kando za barabara nyakati za usiku.
Kwa watu walio mijini ni jambo la kawaida kukuta vyakula vinauzwa pembeni mwa barabara nyakati za usiku. Hii ni biashara ambayo ni rahisi na unaweza kuifanya na haihitaji mtaji mkubwa. Unaweza kupika chips, mishikaki na vyakula vya kawaida, hapa unachohitaji ni kupata eneo ambalo watu wengi hupita mara kwa mara.

Monday, April 15, 2019

Funguka akili sasa ili kutoka kimaisha


By Diana Morsad
Uzoefu unaonyesha kuwa biashara nyingi zilizoanzishwa na wafanyakazi ambao wakati mwingine huwa na elimu ya biashara hufa mapema au hufanya vibaya kwa muda mrefu.
Wapo wafanyakazi huingiza fedha nyingi kwenye biashara na kuishia kukata tamaa kujiingiza kwenye biashara.

Wakati yako masomo mengi ya biashara yanayofundishwa darasani, ukienda kufanya biashara kwa vitendo utagundua kuna elimu nyingine ya biashara inayopatikana huko mtaani haiko kwenye vitabu vyovyote ulivyovisoma na kutunukiwa cheti ulichonacho.
Elimu hii ya mtaani huwa haipatikani bure, kuna gharama zake pia, ingawa gharama hizo huwa hazionekani moja kwa moja. Gharama hizo ni pamoja na kupata hasara, kupoteza muda kubadilisha biashara mara kwa mara na wakati mwingine hata msongo wa mawazo.
Baadhi ya makosa ambayo wafanyakazi huyafanya wanapoanzisha biashara zao ni haya yafuatayo:
Kuanzisha biashara wasizozijua
Unakuta watu wamekaa wanasema biashara ya kuuza chakula inalipa sana, unaona wateja walivyo wengi pale kwa mama Ashura. Wote hawa wanaoshauriana hawajawahi kuwa na biashara kama hiyo na wala hawajui undani wa biashara yenyewe. Mara utasikia mmoja wao anataka kufungua biashara kama hiyo.
Kabla ya kuanzisha biashara ni vyema sana ukatumia muda wako kujifunza hiyo biashara hususani kutoka kwa wanaoifanya. Tena, usijifunze mambo mazuri tu ya hiyo biashara jaribu kudodosa na changamoto zake.
Ukipata bahati ya kushiriki kwenye hiyo biashara moja kwa moja kama kushinda hapo kwenye biashara ya mwenzako na kuona biashara ilivyo utaweza kujifunza mengi zaidi.
Wanaozifanya hizo biashara hata kama hawana elimu
kama ya kwako, ukikubali kushuka chini ujifunze kwao utagundua kuwa watu hawa huwa na vitu vingi sana vya kukufundisha walivyojifunza mtaani.
Nimeona baadhi ya wafanyakazi wenye biashara zao hata wakipita karibu na majirani zao kwenye biashara hawawasalimii. Usipozungumza na hawa watu ambao wao ndiyo huwa wanashinda huko sokoni, unategemea utawezaje kupata taarifa za yanayojiri mjini.
Kuna wakati inakubidi utumie hata fedha ili kufanya utafiti wa kina wa upatikanaji wa bidhaa, ufungashaji na upatikanaji wa masoko. Hii itakusaidia kupata picha halisi ya biashara unayotaka kwenda kuianzisha.
Kutokuwa na muda na biashara zao
Ni mara chache sana unaweza kumuachia uliyemuajiri asimamie biashara yako na akafanya kazi kama ambavyo unataka wewe. Ikitokea umepata mtu ambaye anaweza kusimamia biashara yako kama ambavyo ungefanya wewe, ni kwa bahati sana. Mara nyingi sana biashara ili ifanikiwe lazima mwenye biashara awe na muda nayo.
Utakayemuajiri hatawasikiliza na kuwajibu wateja kama ambavyo ungefanya wewe, wakati mwingine hatauza bidhaa kwa bei ambayo ungeuza wewe. Tena hatatuza fedha kwa makini kama ambavyo ungefanya wewe.
Hata kama umebanwa na kazi yako kama hauna muda na biashara utakayoianzisha ni bora usiianzishe.
Tenga muda hata wa jioni kwenda na wewe kukaa hapo kwenye hiyo biashara ujifunze na kuona mambo yanavyokwenda. Wakati mwingine ukiweza ukae siku nzima uwahudumie wateja, uwasimamie watenda kazi wako.
Ukiwa unatenga muda kwa ajili ya biashara yako itakusaidia wewe kuifahamu kwa undani, kujua aina ya wateja unaowahudumia na mahitaji yao, wakati mwingine utajua hata mambo ambayo yanafanyika wakati wewe haupo.
Imani potofu kuwa biashara ni rahisi
Mtazamo wa haraka haraka wa wafanyakazi wengi ni kuwa biashara sio ngumu sana. Hawajui kwamba biashara ina changamoto zake na ni safari inayohitaji juhudi na kujitoa.
Baadhi yao wanajua kuwa ina changamoto ila kiasi cha changamoto wanachokipimia ni kidogo kuliko changamoto halisi za kibiashara.
Wakati mwingine utawaona maofisa wa serikali wakidai tozo kubwa kwa biashara ndogo sana. Kwa harakaharaka ukisoma mtazamo wao utagundua hawajui mazingira halisi ya biashara.
Inawezekana ukaona matunda ya biashara yako kwa haraka ila mara nyingi sana inahitaji uwekezaji wa muda mrefu, uvumilivu na kujifunza. Ukweli ni kuwa wengi tunafanya biashara ili tupate faida, ila tatizo la waajiriwa ni imani kwamba watawekeza leo watapata faida kubwa kesho.
Faida ni zawadi aipatayo mfanyabiashara kwa kuweza kuvumilia, kutoa muda wake, na kutumia rasilimali alizo nazo vizuri kutoa huduma bora kwa jamii.
Maana yake ni kwamba kiasi cha uvumilivu, muda utakaoutumia na rasilimali zingine ndiyo vinavyoamua kiasi cha faida. Ukiongeza uvumilivu, ukiongeza muda unaoutumia kwenye bishara yako, ukiongeza mtaji na ujuzi wa biashara utaweza kuongeza faida.
Kusahau gharama ya kujifunza biashara
Ni uhalisia ya kwamba kila anayeanzisha biashara anatamani asipate hasara. Ila uhalisia mwingine pia ni kuwa hasara kwa baadhi ya nyakati kwenye biashara haziepukiki. Hasara ni ishara kwamba kuna jambo haukulifanya sahihi. Hii inaitwa gharama ya kujifunza.
Hasara huwa inakusababisha uanze kuitazama biashara yako kwa upya tena. Unaanza kujiuliza maswali ya kwanini ulipata hasara? Yawezekana eneo uliloanzisha biashara yako sio eneo sahihi, wateja hawana uhitaji mkubwa wa bidhaa unazouza, bei unayouza sio rafiki kwa aina ya wateja uliowalenga na mambo kama hayo. Maswali haya hukusababisha uanze kudodosa zaidi kwa watu wengine.
Hasara huwanyenyekeza wenye kiburi, huongeza ufanisi kwenye utoaji wa huduma na umaridadi kwenye utengenezaji wa bidhaa. Wateja huanza kupewa thamani inayostahili. Jambo la kuzingatia ni kwamba wafanyakazi wasikate tamaa wanapoanza biashara na kupata hasara. Hakuna sababu ya kuacha biashara na kugeukia maisha mengine.
Ni lazima kuelewa kwamba kila jambo zuri lina gharama zake. Fedha utakazozitoa na kuziwekeza ni gharama mojawapo, ila hasara iweke pia kwenye mpangilio wako. Isikukatishe tamaa. Jifunze na uitumie kama fursa kupiga hatua zaidi.

Monday, April 8, 2019

Sambusa za nyama













Mahitaji

  • Nyama steki kilo 1 
  • Vitunguu maji 2
  • Majani ya Giligiliani vifungu 2 
  • Garam masala kijiko 1 cha chai
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
  • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
  • Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
  • Karoti 2 kubwa
  • Pilipili hoho 2
  • Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
  • Manda
  • Butter 

    Maelekezo

    • Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
    • Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
    • Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
    • Chukua frying pan pana, weka butter. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
    • Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
    • Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala koroga dakika 2, epua. Usiifunike
    • Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
    • Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
    • Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
    • Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia kisha unaepua zinakuwa tayari kwa kuliwa

Sunday, March 31, 2019

Nini ufanye kabla ya kuchagua wazo la biashara

Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii.
Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.
Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.

1. Chagua wazo unalolipenda

“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”
Marsha Sinetar
Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya.
Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.
Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.

2. Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu

Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.
Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

3. Zingatia swala la fedha

Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.
Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

4. Angalia uhitaji wa soko

Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.
Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

5. Ushindani

Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.
Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza.
Neno la mwisho
Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa. Ni muhimu ukahakikisha kuwa wazo unalolichagua unalimudu vyema na linaweza kukupa faida ya uhakika katika eneo unalolilenga.
Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako

Wednesday, March 27, 2019

Ice cream za shilingi mia tu zinaweza kukutoa kimaisha











Mahitaji 
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ Maji lita 7 
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote) 
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza) 
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)

HATUA: 
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch au ubuyu na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu. 

Wednesday, March 13, 2019

Namna ya kuandaa juice yenye mchanganyiko wa maembe na karoti.


 By Diana Morsad

Wapendwa wangu unaangaika buree na maisha magumu, umesha choka sana kuzunguka na mavyeti yako katika maofisi meeengi bila mafanikio, unasubiri nini wakati ajira zipo mikononi mwako kwa mtaji mdogo sana unaweza kukutoa kimaisha changamkia fursa sasa wacha kulala.




UTAYARISHAJI WAKE

Chukua maembe 5 au kiasi chako, chukua karoti 3, tangawizi kidogo,
kisha anza kuviosha kwa maji ya uvuguuvugu, weka kwenye sahani na
anza kumenya hayo matunda yako kwa usafi wa hali ya juu sana.
ukimaliza andaa blender, sukari kiasi kidogo sana

b) Anza kumenya vipande viodogo vidogo vya maembe weka kwenye
bakuri kisha menya karoti vipande vigodo vichanganye kwenye maembe
chukua tangawizi kidogo sana imenye na changanya na hayo matunda

c) Chukua blender yako weka hayo matunda mchanganyiko weka na maji
yaliyochemsha kiasi kidogo kisha anza kusaga matunda yako 
hakikisha kuwa yanakuwa malaini sana kisha chuja pembeini kwenye
bakuli, weka sukari kidogo sana kama vijiko 5 vya chakula
koroga koroga mpaka ilainikie kwenye matunda hayo kisha weka kt
jagi lako na weka hiyo juice kwenye friji ili iwe baridi kiasi

Tayari umeshapata juice yenye mchanganyikko wa maembe na karoti
inafaa kunywa na mikate, keki, au chochote utatakachojisikia kunywa
nacho, na pia unaweza ukaiuza mahali popote pale kwa ujasiri wote kutokana na uwepo wa radha nzuri ya juice hiyo.
By Diana Morsad




Habari zenu wapendwa wangu usikate tamaa hata Mimi nilihangaika kweli kujifunza mapishi ya ubuyu saaanah, kiukweli.nilishaharibu sukari yangu Mara kibaooooo laikn sikuchoka. Sasa ni hivii


















Mahitaji:
Sukari kilo moja
Ubuyu vikombe 6
Unga wa ubuyu kikombe kimoja
Pilipili manga kijiko kimoja
Ikili kiasi
Bikabonet of soda kijiko kimoja flat
Maji kikombe kimoja
Rangi nyekundu kijiko kimoja
Harufu yyte utayopenda

Kupika sasa:
Chambua ubuyu wako..Pima vikombe 6 vya nusu kilo tia kwenye bakuli kubwakubwa, tia pamoja na iliki yako na pilipili manga...tia sukar kwenye sufuria na maji kikombe kimoja(kile kile kikombe cha nusu)...bandika jikoni tia na rangi yako..acha vichemkeeee( hapa kwenye sukari watu wengi wanakosea)...sukari inatakiwa iive ili ubuyu uweze kukauka! Sukari icpoiva ubuyu haukauki ng'ooooo!

Utajuaje km sukari imeiva???? Sukari ikichemsha inakawaida kutoa povu inaweza kumwagika! Hapo inakuwa haijaiva...ukioona inachemka INA povu lkn haipandi juu jua kuwa imeivaaaa!!! Yana linachemka putu!putu!putu!!

Epua sukari mimina kwenye bakuli uliloweka ubuyu! Km una harufu yako nyingine wekaaaa...koroga ubuyu mpaka ukorogeke! Tia b/soda endelea kukorogaaa utauona km unavimbavimba hivi...tia ungawako was ubuyu kiss cha kikombe kimoja kilekile cha nusu! Korogaaaa...unaweza ukakauka hapo au ukaufunika mpaka baada ya nusu SAA...ubuyu wako utakuwa upo tayariiii....

Jaribuni kupika mpenwa wangu kisha rudi tena hata kunipa maji 
NB: Hakikisha unafuata kila hatua.

Tuesday, March 12, 2019

Jifunze Kupika Karanga za Mayai kwa Ajili ya Kuuza.





Mahitaji

Karanga kilo 1
Yai moja
Mafuta ya kula ( ya maji ) mls 750
Sukari vijiko 6 vya chakula
Unga wa ngano kikombe kimoja cha kahawa( coffee cup)
Chumvi ya unga nusu kijiko cha chai.
Jiko
Chombo –Sufuria/bakuli
Mwiko /kijiko kikubwa

Maelekezo

Chukua  yai,  pasua  na  koroga  kwenye  chombo  kisafi.
Chukua  karanga,mimina kwenye chombo ulicho koroga yai ,changanya kwa kutumia mikono.
Weka chumvikidogo, changanya vizuri, weka sukari changanya, mimina unga wa ngano, changanyavizuri.
Weka mafuta jikoni hadi yapate moto.
Chota karanga kwa kutumia kijiko  kikubwa  na  weka  kwenye  mafuta  kisha  zigeuze  bila  kuacha  hadi utakapoona karanga zimebadilika rangi kua kahawia.
Tumia  kijiko  kikubwa  kuziepua  na  weka  kwenye  chombo  kisafi  cha  wazi  ilizipoe.
Funga kwenye vifuko vidogo na zihifadhi mahali pasafi tayari kwa kula au kuuza. 

Biashara ndogo ndogo zinazoweza kukuletea faida kwa haraka

By Diana Morsad
Biashara ni kazi yoyote ambayo lengo lake kuu ni kupata faida lakini wakati mwingine badala ya faida tunapata hasara. Mfanyabiashara yeyote ni mjasiriamali(Risk taker) ambae anatoa pesa yake ili kuanzisha biashara bila kujali kuwa anaweza pata hasara. Aina za ujasiliamali, kuna wajasilimali wakubwa na kuna wajasiliamali wadogo hii hutokana na kiwango cha mtaji ambao mjasiliamalia anakuwanacho kwa ajili ya kuanzisha biashara.

Maswali kubwa ambalo wajasiriamali wote huwa wanapata mwanzoni ni mengi sana mfano, fursa zipi zipo katika jamii?, aina za biashara nazoweza anzisha katika mazingiza husika, fursa za biashara katika wakati huu?, na wajasiliamali wengi hupenda biashara yenye faida ya haraka, pia hupenda biashara yenye faida kubwa.

Baada ya tafiti mbali mbali nilizofanya katika maeneo mbali mbali nimegungua hizi aina za biashara ndogondogo zenye faida ya haraka na faida kubwa, ambazo ni fursa kwa mtu yeyote mwenye nia kabisa ya kutoka hatua alionayo kwenda hatua kubwa zaidi hata kama anamtaji kwanzia elfu kumi (10000Tshs) au 5$ mtu anzaweza kuanzia kama mwanzo wa kufikia malengo yake makubwa.
nn
1. Biashara ya matunda

Hii ni biashara ya kununua na kuuza matunda kwa walaji wa mwisho, watu wengi hupenda matunda hivyo uhitaji wa matunda ni mkubwa na soko lake nilauhakika zaida. Hii ni fursa kubwa kwa watu wote katika maeneo mbalimbali, mara nyingi matunda huwa na faida ya hadi asilimia hamsini za gharama yake ya manunuzi. Kama wewe ni mkazi wa Dar es salaam unaweza ukawa unaenda buguruni kununua matunda harafu unaenda kuuza kwenye maeneo unayo ishi. Mtaji wa matunda ni mdogo sana hata unaweza anza na elfu 20 kama una eneo zuri la kuuzia. Sio kwa wakazi wa Dar tu ila nimetoa mfano ila kila sehemu za Tanzania kunamaeneo watunda yanapatikana kwa bei nzuri, hivyo ni fursa kwa mjasuliamali mdogo kuanza biashara hii na baada ya muda kuna uhakika mkubwa sana wa tupata faida kubwa na haraka. Angalizo biashara hii haihitaji tamaa maana niyavitu vinavyo haribika kwa muda mfupi hivyo inapaswa ulete mzingo kulingana na idadi ya wateja wako katika soko.

2. Biashara ya karanga za mayai

Kama kuna aina ya biashara ndogondogo rahisi na inafaida kubwa na ya haraki ni hii. Kwanza haiitaji mtaji mkubwa kuweza kuanzisha hata kama una elfu kumi tu unaweza anzisha na ikasonga mbele, kwa kiasi cha kilo moja ya karanga, unga wa ngano robo, sukari robo, mafuta lita moja na mayai mawili biashara inaanza. Soko lake ni lauhakika maana watu wengi wanapenda vitamu. Kama unamtaji mkubwa unaweza ongea na watu wa kwenye maduka harafu ukawa unawauzia kwa jumla nawao wanauza, kama utapata wateja wa kutosha hii haitakuwa biashara mdogo tena bali biashara kubwa na yenye tija, kiwango chake cha faida huanzia asilimia 25% za gharama za manunuzi. Pia faida nyingine ya biashara hii hata kama unashughuli nyingine unaweza ukafanya wakati umetoka kazini au shuleni ukatengeneza na ukasambaza kwa wauzaji wa maduka.

3. Biashara ya bisi(popcorn)

Kutokana wa watu wengi kupenda popcorn biashara hii imekuwa na tija kubwa maada soko lake nilauhakika na ni kubwa. Kama ukibata sehemu nzuri yenye idadi kubwa ya watu unaweza ukawa unapata mpaka zaidi ya shiling elfu 30 kwa siku moja. Biashara hii inahitaji mtaji wa kama laki tano kuanza maana machine nyingi za popcorn huanzia laki tatu mpaka laki tano kulingana na aina ya mashine na ubora wake. hii si kama biashara nyingine ndogondogo inahitaji kujipanga kwa kiasi fulani ili kuweza ianzisha lakini inafaida nzuri sana maana siku hizi popcorn haziliwi na watoto tu bali na kila mtu.

4. Biashara ya juisi

Mtaji wa elfu 60 unatosha kabisa kuweza anzisha biashara hii na ikawa na tija kuwa. Si lazima uwe na eneo la kuuzia ndio uweze anzisha biashara hii bala ni utajari ku wakufanya ndio unahitajika, Njia bora zaidi ya kufanya biashara hii nikwakutembeza mtaani, kwenye maofisi, kwenye maduka, chuoni na sehemu mbalimbali, hii ni biashara ambao wajanja wato wanaopenda kazi wanaitumia kama mwanzo bora kuliko kukaa mtaani au vijiweni kupiga stori siku nzima, kama mtu ukiwa na nia hii ni biashara bora na yenye tija na faida kubwa hivyo ni fursa nzuri ya kibiashara ya kuanzia. Kwa wanaoanza unaweza anza na brenda ya kawaida ya elfu 30 inatosha kwa mwanzo, na matunda unatakiwa kununua kwa wauzaji wa jumla ndipo utapata faida nzuri zaidi.

5. Kuuza nguo kwa kutembeza

Kama unamtaji mdogo unaweza kuwa unaenda kuchambua nguo nzuri mtumbani harafu unakuja kutembeza kwa watu mtaani na kunywe majumba. Si lazima ziwe za mtumba ila hata za special. Asili ya wanadamu ni uvivu hivyo kama mjasiliamali hiyo ni fursa kwako ya kutumia uvivu wa mwanadamu kama chanzo cha kipato chako. Nguo huwa zinafaida sana pia unaweza ukawa unawakopesha kwa ongezeko la bei wanakuwa wanalipa kidogokidogo. Biashara hii ni nzuri sana hata kwa watu wanaoishi mikoani unaweza ukawa unachukua mziko wako kama ni Dar au kwa kanda ya ziwa Katoro na unakuja kutembeza sehemu unayoishi, haihitaji ofisi wala haihitaji mbwembwe.

6. Biashara ya kuuza maji

Kwa yeyote ambae anafikilia kwa kina anaweza tambua kuwa biashara ya kuuza maji kwa sehemu zenye shida ya maji ni bonge la dili. Sehemu nyingi zenye shida ya maji, maji huuzwa kwanzia shiling 500 za kitanzania mpaka shilingi 1000 kwa dumu la lita 20, na wauzaji hununua kwa wasitana bei ya shilingi 100 hadi 300 kwa dumu. Kama ukipiga hesabu za haraka haraka unaweza ukagungua ni jinsi gani biashara hiyo ilivyo na faida nzuri. Na uache kujifunza kwa walio shindwa, jifunze kwa waliofanikiwa na si lazima mtu fulani akifanya biashara fulani akashindwa kuwa nawe utashidwa ni mawazo yakivivu hayo.

7. Huduma ya kutunza watoto wadogo

Kutokana na vitendo vya ukatili na ukosekanaji wa wafanya wa ndani, watu wengi wenye watoto wamekuwa wakipata wakati mgumu sehemu ya kuacha watoto wao katika mazingira salama. Hivy kama huna mtaji ni nzuri kuanzisha biashara ya kituo cha kutunza watoto wadogo wakati wa mchana wakati wazazi wao wakiwa katika shughuli za maisha.

8. Kufundisha

Kama unaelimu yako nzuri juu ya vitu fulani mfano mapishi, kilimo, ufugaji, afya au biashara, unaweza ukafungua darasa kwaajili ya kufundisha watu juu ya vitu vinavyohusu taaluma yako na wakawa wanalipoa feza kwa ajili ya hiyo elimu unayo wapa,

Pia unaweza fundisha tuition center kutikana na uhitaji mkubwa wa sasa wa wazazi kupenda watoto wao wawe wanapata masomo ya ziada.

Monday, March 11, 2019

Ni rahisi tu, unaweza kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji


By Diana Morsad. LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.


Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Thursday, March 7, 2019












Barani Afrika idadi ya vijana kama ilivyo katika mabara mengine inaongezeka kila uchao. Kasi ya ongezeko hilo haiendi sambamba na mabadiliko ya stadi shuleni ili waweze kupata ujuzi wa kuwawezesha kukabiliana na maisha yao. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda, UNIDO limeanzisha mradi wa kujumuisha mtaalamu wa ujasiriamali katika shule za msingi na sekondari barani Afrika. Miongoni mwa nchi zilizoanza kunufaika na mradi huo ni Msumbiji.